KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester United, Shinji Kagawa amebainisha kuwa anatakiwa kuimarisha kiwango chake la sivyo atashindwa kudumu katika timu hiyo yenye maskani yake Old Traford. Nyota huyo wa kimataifa wa Japan alifanikiwa kuanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya West Bromwich Albion Jumamosi iliyopita lakini alitolewa katika kipindi cha mapumziko. Kagawa amepangwa mara nne pekee katika kikosi cha Moyes msimu huu na amekiri kwamba anatakiwa kujiimarisha kama anataka kubakia hapo. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 amesema anajua bado ana safari ndefu ya kuhakikisha anakuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza lakini haweza kukata tama kuhakikisha anafikia malengo yake.
No comments:
Post a Comment