MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Mario Gotze amekiri kuwa anazidi kuchanganyikiwa kuhusiana na suala la kukaa nje ya uwanja na ana hamu kubwa ya kurejea tena katika kiwango chake. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umriwa miaka 21 amecheza mechi tatu pekee akiwa na Bayern toka ajiunge nao akitokea Borussia Dortmund kwa ada ya euro milioni 37 na amekuwa nje ya uwanja toka Agosti baada ya kupata majeruhi katika mchezo Supercup dhidi ya Chelsea. Gotze amesema sio jambo rahisi kuendelea kuvumilia kwasababu kila mchezaji anapenda kucheza kila dakika na kila mchezo. Nyota aliendelea kusema kuwa hilo haliwezi kumkatisha tamaa kwasababu atapambana kuhakikisha anakuwa na namba ya kudumu katika kikosi hicho kinachonolewa na Pep Guardiola.
No comments:
Post a Comment