NAHODHA wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard amesema alikuwa na hofu mshambuliaji nyota wa timu hiyo Luis Suarez angeondoka katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi. Suarez mwenye umri wa miaka 26 aliomba kuondoka Anfield na alikuwa akihusishwa kwenda katika vilabu vya Arsenal na Real Madrid. Gerrard amesema timu inapokuwa na mchezaji mzuri kama Suarez ni wazi kuwa vilabu mbalimbali vitakuwa vikimuwinda ndio maana alikuwa na hofu ya nyota huyo kuondoka. Suarez alirejea uwanjani katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Manchester United baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi 10 kwa kumuuma mkono Branislav Ivanovic.
No comments:
Post a Comment