Tuesday, October 29, 2013

MOURINHO KUREJEA CHELSEA HALIKUWA JAMBO LA KUSHANGAZA.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa hakushangazwa kuona Jose Mourinho akirejea katika klabu ya Chelsea, kauli ambayo imekuja wakati ambapo wawili wanatarajia kukutana tena katika mchezo wa Kombe la Ligi itakayofanyika Uwanja wa Emirates baadae leo. Arsenal wameshinda mechi zao tisa kati ya 10 walizocheza katika uwanja wao wa nyumbani lakini Wenger bado hajawahi kuifunga timu ambayo inanolewa na Mourinho. Wakati Mourinho alipotua Chelsea kwa mara ya kwanza alikuwa akiingia katika mzozo wa mara kwa mara na Wenger lakini meneja huyo alisistiza kuwa hilo sio tatizo tena na ana furaha kumuona amerejea tena. Wenger amesema halikuwa jambo la kungaza kumuona kocha huyo amerudi kwasababu ni suala ambalo lilikuwa likizungumziwa mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment