Tuesday, October 29, 2013

VAN PERSIE AMTABIRIA MAKUBWA JANUZAJ.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester United, Robin van Persie anaamini kuwa mchezaji mwenzake anayechipukia Adnan Januzaj ana uwezo wa kuja kuwa mmoja wa wachezaji bora kabisa duniani. Kinda huyo mwenye miaka 18 ameanza vyema msimu huu kwa kuisadia United kutoka nyuma na kushinda mchezo dhidi ya Sunderland mapema mwezi huu huku akisaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo. Akihojiwa Van Persie amesema binafsi ni mshabiki wa kinda huyo na anadhani ana kitu za ziada kitakachomfanya kuwa nyota baadae. Van Persie aliyeondoka Arsenal mwaka jana kujiunga na United aliendelea kudai kuwa kwa miaka kadhaa ameshuhudia wachezaji mbalimbali vijana wanavyoibuka hivyo hana shaka kwamba Januzaj atakuja kuisaidia United kiasi kikubwa katika siku za usoni.

No comments:

Post a Comment