Tuesday, October 29, 2013

FERNANDINHO AIPA NAFASI BRAZIL KUNYAKUWA KOMBE LA DUNIA.

KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Brazil, Fernandinho ameipa nafasi timu ya taifa ya nchi hiyo kunyakuwa taji la Kombe la Dunia mwakani litakalofanyika katika ardhi ya nchi yao. Uhamisho wake kwenda Ligi Kuu ya Uingereza katika klabu ya Manchester City akitokea Shakhtar Donetski umechukuliwa kama sehemu ya kunyanyua nafasi yake kama mchezaji wa kati katika timu ya taifa. Ambapo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 anadhani michuano hiyo kuchezwa katika ardhi ya nyumbani kwao ni nafasi nzuri kwao kubakisha taji hilo hapohapo. Fernandinho amesema kucheza mbele ya mashabiki wa nyumbani ni kitu ambacho hakijashuhudiwa kwa kipindi kirefu hivyo itakuwa ni nafasi ya kuonyesha ubora wao.

No comments:

Post a Comment