Tuesday, October 29, 2013

FLETCHER AREJEA TENA UWANJANI BAADA YA KUKOSEKANA KWA MIEZI 10.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester United, Darren Fletcher amevaa jezi ya klabu hiyo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 10 iliyopita baada ya kupoana vidonda vya tumbo vilivyokuwa vikimsumbua. Fletcher ambaye alikosa mechi nyingi msimu uliopita baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa vidonda vya tumbo vilivyokuwa vikimsumbua alicheza dakika 67 katika mchezo wa vijana wa chini ya umri wa miaka 21 dhidi ya Fulham ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Fletcher alianza mazoezi rasmi katikati ya Septemba na muda si mrefu anaweza kurejea katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kama hali yake ikiimarika. Katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa AJ Bell uliopo Salford ulishuhudiwa na wengine wa zamani wa United kama David Beckham, Phil Neville na Nicky Butt.

No comments:

Post a Comment