Thursday, October 31, 2013

MADRID YAMNYEMELEA BENZEMA.

KLABU ya Real Madrid inajipanga kwa usajili wa dirisha dogo mwezi January kutumbukia kumnasa Luis Suarez wa Liverpool kwa dau la paundi milioni 20 pamoja na mshambuliaji Karim Benzema. Suarez bado inaelezwa anataka kuondoka Anfield, licha ya mwanzo mzuri wa msimu kwa Liverpool. Arsenal nao wanajipanga kwa dau lingine baada ya kutolewa nje kwenye usajili uliopita wa majira ya joto. Lakini Suarez inaonekana anapenda zaidi kwenda Real Madrid inayofundishwa na Carlo Ancelotti na wakali hao wa Hispania wana matumaini ya kuwashawishi Liverpool kwa kuwapa fedha na mchezaji mwenye jina kubwa Benzema.

No comments:

Post a Comment