Thursday, October 31, 2013

ANCELOTTI AMPONGEZA BALE.

KOCHA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amesifu mchango wa Gareth Bale ambaye alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 7-3 iliyopata timu hiyo dhidi ya Sevilla jana. Katika mchezo huo Bale alianza kwa mara ya kwanza toka atue Santiago Bernabeu ambapo ndiye aliyefunga bao la kuongoza katika dakika ya 13 kabla ya kufunga bao lingine kwa adhabu ndogo. Mabao mengine ya Madrid yalifungwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga matatu na Karim Benzema aliyefunga mawili. Ancelotti amesema alicheza vyema na kuonyesha kipaji cha hali ya juu alichonacho pamoja na kwamba imechukua muda kurudi katika kiwango chake kutokana na majeruhi ya mara kwa mara yaliyokuwa yanamsumbua.

No comments:

Post a Comment