Thursday, October 31, 2013

FIFA YAIRUHUSU MISRI KUTUMIA UWANJA WAKE WA NYUMBANI.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeruhusu timu ya taifa ya Misri kucheza mchezo wake wa mkondo wa pili wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ghana katika jijini la Cairo pamoja na hofu ya hali ya usalama. Chama cha Soka cha Ghana-GFA kilituma maombi FIFA ya kutaka kutafutwa uwanja mwingine ambao utakuwa salama kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika Novemba 19 mwaka huu. Hata hivyo, FIFA ilithibitisha jana kuruhusu mchezo huo uchezwe jijini Cairo baada ya wakaguzi kuhakikisha hali ya usalama. Mshindi katika mchezo huo wa mtoano atafuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment