MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema beki mahiri wa kulia wa timu hiyo, Bacary Sagna atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu kutokana na majeraha ya msuli wa nyuma ya paja yanayomsumbua. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa alipata majeraha hayo Jumanne wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli ambao Arsenal ilishinda kwa mabao 2-0. Sagna anatarajiwa kukosa mechi za ligi dhidi ya West Bromwich Albion Jumapili hii na Norwch City itakayochezwa Octoba 19 pamoja na mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Finland Octoba 15. Mbali na mechi hizo Sagna pia ataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Arsenal Na Borrusia Dortmund Octoba 22 mwaka huu.
Friday, October 4, 2013
SAGNA NJE WIKI TATU.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment