Thursday, October 3, 2013

MJADALA WA QATAR 2022 KUCHUKUA NAFASI KUBWA MKUTANO WA FIFA ZURICH.

RAIS wa Shirikisho la Soka Dunia-FIFA, Sepp Blatter anakabiliwa na upinzani kuhusu mpango wake wa kubadilisha michuano ya Kombe la Dunia 2022 itakayofanyika nchini Qatar kuchezwa katika majira ya baridi. Mapema mwezi Agosti Blatter amesema anataka kuhamisha michuano hiyo ili kuepuka joto kali linaloweza kufikia nyuzi joto 40 katika majira ya kiangazi. Hata hivyo wajumbe watatu wa kamati ya utendaji ya FIFA wamedai kuwa watapingana na maamuzi yoyote ya haraka yatakayofanyika kuhamisha michuano hiyo. Naye rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini amesema itakuwa ni suala lisilowezekana kupigia kura suala hilo wakati watakapokutana kulijadili baadae leo. Mkutano huo wa siku mbili utakaofanyika jijini Zurich, Switzerland utahudhuriwa na wajumbe wapatao 28.

No comments:

Post a Comment