GABON imetangaza jana kutuma maombi ya kuomba kuandaa michuano ya 32 ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019 na kuthibisha tuhuma zilizokuwa zimezagaa kwa kipindi kirefu. Kwa mujibu wa Wizara ya Michezo ya nchi hiyo maombi hayo yalitumwa Septemba 30 wakidai kuwa tayari nchi hiyo ina miundo mbinu ya kutosha iliyotumika kwa ajili ya michuano hiyo mwaka 2012 ambayo iliandaliwa kwa pamoja na Equatorial Guinea. Hata hivyo Gabon watapata upinzani mkali kutoka kwa Algeria, Ivory Coast na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao nao tayari wameshatuma maombi yao. Katika taarifa yake wizara hiyo ilitamba kuwa nafasi kubwa ya kulishawishi Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kutokana na mafanikio waliyopata kwenye michuano ya 2012.
No comments:
Post a Comment