MCHEZA tenisi nyota wa Hispania, Rafael Nadal amepiga hatua nyingine kusogelea nafasi ya kwanza katika orodha za ubora wa mchezo huo duniani baada ya kupambana na kushinda dhidi ya Philipp Kohlschereiber katika michuano ya wazi ya China. Nadal mwenye umri wa miaka 27 alishinda kwa alama 6-4 7-6 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo ambapo sasa atakwaana na Fabio Fognini wa Italia. Nadal atachukua nafasi ya kwanza inayoshikiliwa na Novak Djokovic kama akitinga fainali ya michuano hiyo au Mserbia huyo akishindwa kushinda taji hilo. Kwa upande wa wanawake Agnieszka Radwanska anashika namba tatu, Li Na anayeshika namba nne na Petra Kvitova anayeshika namba tisa wote walishinda mechi zao na kusonga mbele katika michuano hiyo inayofanyika jijini Beijing.
No comments:
Post a Comment