KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta ameonyesha nia yake ya kumalizia soka lake akiwa na klabu hiyo na kumaliza utata uliozagaa kuwa hataweza kuongeza mkataba wake. Tetesi za kuondoka kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 ziliibuka baada ya tuhuma kuwa alikataa kuongeza mkataba na klabu hiyo. Hata hivyo Iniesta ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2015 amesema ana ndoto za kumalizia soka lake hapo hivyo hana shaka kwamba ataongeza mkataba wake wakati utakapofika. Iniesta amesema amekuwepo Barcelona toka akiwa na umri wa miaka 12 na ndoto zake ni kustaafu soka akiwa hapo.
No comments:
Post a Comment