MENEJA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema klabu hiyo itajirudi baada ya kuanza vibaya na kushinda taji la Ligi la Kuu nchini Uingereza pamoja na kuwa nyuma ya vinara Arsenal kwa alama nane. Ushindi mara mbili iliyopata United katika mechi zao tatu zilizopita inamaanisha kuwa timu hiyo inayonolewa na David Moyes imeanza kurejea katika kiwango chake cha kawaida. Ferguson mwenye umri wa miaka 71 amesema United imewahi kuanza vibaya mara nyingi lakini ndio timu pekee inayoweza kutoka nyuma na kushinda taji la ligi kwasababu ya historia yao. Ferguson ambaye ambaye amebakia kama mkurugenzi wa klabu hiyo, alistaafu nafasi ya ukocha mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kushinda mataji 38 katika miaka 27 aliyokuwepo hapo.
No comments:
Post a Comment