Tuesday, October 29, 2013

MESSI, RIBERY, RONALDO WAONGOZA ORODHA YA BALLON D'OR.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetoa orodha ya wachezaji 23 watakaogombea tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or. Miongoni mwa wachezaji waliopo katika orodha hizo ni pamoja na Lionel Messi ambaye anashikilia taji hilo aliloshinda mwaka jana, Franck Ribery wa Bayern Munich na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid. Bayern ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu uliopita ndio waliotoa wachezaji wengi zaidi katika orodha hiyo ambapo mbali na Ribery pia wapo Philipp Lahm, Thomas Muller, Manuel Neuer, Arjen Robben na Bastian Schweinsteiger. Mapema Mwezi Desemba mwaka huu FIFA na France Football watatangaza orodha ya majina matatu watakaopata kura nyingi zaidi kabla ya mshindi wa tuzo hiyo kutangazwa katika hafla itakayofanyika jijini Zurich, Januari 13 mwakani.

Orodha kamili ya wachezaji na timu wanazotoka ni Gareth Bale (Real Madrid), Edinson Cavani (Paris St-Germain), Radamel Falcao (Monaco), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Paris St-Germain), Andres Iniesta (Barcelona), Philipp Lahm (Bayern Munich), Robert Lewandowski (Borussia Dortmund), Lionel Messi (Barcelona), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Mesut Ozil (Arsenal), Andrea Pirlo (Juventus), Franck Ribery (Bayern Munich), Arjen Robben (Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Luis Suarez (Liverpool), Thiago Silva (Paris St-Germain), Yaya Toure (Manchester City), Robin Van Persie (Manchester United), Xavi (Barcelona).

Mbali na wachezaji pia ilitolewa orodha ya makocha watakaogombea tuzo ya kocha bora wa mwaka ambayo ni Carlo Ancelotti (Real Madrid CF), Rafael Benítez (Napoli), Antonio Conte (Juventus), Vicente Del Bosque (Spain), Sir Alex Ferguson (Manchester United's former coach), Jupp Heynckes (Bayern Munich's former coach), Jurgen Klopp (Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Chelsea), Luiz Felipe Scolari (Brazil), Arsene Wenger (Arsenal).

No comments:

Post a Comment