WAZIRI wa michezo wa Brazil, Aldo Rebelo amesema viwanja vyote 12 vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka ujao vitakuwa tayari kwa wakati uliopangwa Desemba mwaka huu. Rebelo aliwaambia waandishi wa habari nchini humo kuwa ana uhakika wa kukamilika kwa viwanj hivyo kwasababu bado hawajachelewa sana. Kauli ya waziri imekuja kufuatia wasiwasi uliokuwepo wa kukamilika kwa wakati kwa Uwanja wa Pantanal uliopo katika mji wa Cuiaba, na kudai kuwa uwanja huo mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 85 hivyo hakuna shaka kwamba utaisha nje ya wakati uliopangwa. Rebelo pia amesema hadhani kuwa michuano hiyo itazongwa na maandamano kama ilivyokuwa michuano ya Kombe la Shirikisho iliyofanyika Juni mwaka huu mwaka huu ambapo waandamanaji walikuwa wakilaumu serikali kutumia fedha nyingi katika michuano hiyo wakati bado huduma muhimu zinapatikana kwa tabu nchini humo.
No comments:
Post a Comment