Monday, October 28, 2013

VETTEL AFIKIA REKODI ZA KINA SCHUMACHER.

DEREVA nyota wa mashindano ya langalanga kutoka timu ya Red Bull Sebastian Vettel ameeleza kuwa na furaha isiyo na kifani baada ya kufanikiwa kunyakuwa ubingwa wa duniani kwa mara ya nne mfululizo kwa kushinda mbio za Grand Prix za India Jumapili. Vettel ambaye ni raia wa Ujerumani anakuwa dereva wan ne kunyakuwa ubingwa huo kwa mara ya nne baada ya Juan Manuel Fangio, Alain Prost na Michael Schumacher na kufanya hivyo katika vipindi vyao. Akihojiwa Vettel amesema amekosa cha kuzungumza kwasababu ni moja ya siku ambazo anafuraha katika maisha yake. Dereva huyo ambaye ameshinda taji hilo huku kukiwa kumebaki mashindano matatu ya kumalizia msimu, aliendelea kudai kuwa imekuwa ni heshima kwake kushindana na baadhi ya madereva bora kabisa wa langalanga.

No comments:

Post a Comment