Monday, October 28, 2013

NILIKATAA KWA MAKUSUDI KUMPA MKONO MOURINHO - PELLEGRINI.

MENEJA wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amesema hakutaka kumpa mkono meneja wa Chelsea Jose Mourinho baada ya kipigo cha mabao 2-1 walichopata. Mourinho aliruka na kwenda kwa mashabiki kushangilia baada ya mshambuliaji Fernando Torres kuifungia Chelsea bao la ushindi katika dakika za majeruhi. Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo Pellegrini amesema hakutegemea kitu tofauti kutoka kwa Mourinho ndio maana akaona haina haja ya kumpa mkono. Mourinho naye alijibu mapigo na kudai kuwa kama kuna mtu anafikiri alifanya vibaya kupanda jukwaani kushangilia na mashabiki anaomba radhi kwa hilo.

No comments:

Post a Comment