Monday, October 28, 2013

HAKUNA HAJA YA WAGHANA KUMTEGEMEA BOATENG - ZAKKOUR.

OFISA mkuu wa zamani wa klabu ya Heerts ya Ghana, Harry Zakkour amewataka mashabiki wa soka wan chi hiyo kumsahau kiungo mahiri wa timu ya taifa maarufu kama Black Stars Kevin-Prince Boateng. Uhusiano wa Boateng na mashabiki wa Black Stars umekuwa mashakani kufuatia jinsi alivyostaafu mwaka 2011 na kurejea tena miezi michache iliyopita lakini mpaka sasa ameshindwa kuichezea nchi hiyo mechi yoyote. Zakkour amesema nchi hiyo ina wacheza nyota wengi wanaoweza kuipeleka mbali hivyo hawana haja ya kuendelea kumuabudu mchezaji mmoja ambaye anaonyesha hana mapenzi nayo. Zakkour aliendelea kudai kuwa hana tatizo lolote na Boateng lakini hadhani kama mchango wake ni muhimu zaidi ya wachezaji waliopo sasa walivyoonyesha. Ghana watatakiwa kung’ang’ania ushindi wao wa mabao 6-1 waliopata dhidi ya Misri katika mechi ya mkondo wa kwanza wakati watakapokwaana tena katika mchezo wa marudiano Novemba 19 ili waweze kujikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014.

No comments:

Post a Comment