KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC imeshapiga hatua moja kufikia fainali ya Kombe la Shirikisho wakati watakapoikaribisha timu ya Stade Malien ya Mali mwishoni mwa wiki hii. Timu hizo mbili zinatarajiwa kukwaana katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili jijini Lubumbashi kesho huku Mazembe wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-1 waliyopata katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa jijini Bamako Octoba 6. Kocha wa Mazembe Patrice Carteron amesema nusu ya kazi tayari wameshafanya lakini bado hawatawadharau wapinzania wao katika mchezo huo. Hata hivyo kuna wingu kubwa limetanda katika mchezo huo kwa Mazembe ambapo hakuna uhakika kama viungo Rainford Kalaba na Nathan Sinkala pamoja na beki Stopilla Sunzu watacheza katika mechi hiyo. Utata huo umekuja kufuatia Shirikisho la Soka la Zambia kutuma malalamiko yao Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa Mazembe kuwakatalia wachezaji kutimiza majukumu yao ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment