Friday, October 18, 2013

OZIL, SAGNA NA CAZORLA WAKO POA - WENGER.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa nyotwa wake Mesut Ozil, Bacary Sagna na Santi Cazorla wote wako fiti kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Norwich City. Kulikuwa na wasiwasi wa nyota hao kukosekana baada ya Ozil kutolewa nje kwa maumivu katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia kati ya Ujerumani na Sweden wakati Sagna na Cazorla wenye walikuwa majeruhi kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa. Lakini Wenger aliwaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kudai kuwa nyota hao pamoja na kikosi kizima cha timu hiyo wako fiti tayari kwa mchezo huo wa Jumamosi. Cazorla ambaye alikuwa majeruhi kwa muda alianza kufanya mazoezi rasmi na timu hiyo wakati wa mapumziko wa mechi za kimataifa.

No comments:

Post a Comment