Friday, October 18, 2013

DROGBA ATUNUKIWA TUZO YA GOLDEN FOOT.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba ametunukiwa tuzo ya Golden Foot jijini Monaco, Ufaransa. Drogba mwenye umri wa miaka 35 ambaye anakipiga katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki alipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mwana wa Mfalme wa Monaco tuzo ambayo hutunukiwa wachezaji wenye umri wa miaka 28 na zaidi ambao bado wanacheza. Nyota huyo pia anakuwa mchezaji wa pili aliyecheza katika Ligi Kuu nchini Uingereza kutunukiwa tuzo hiyo baada ya Ryan Giggs wa Manchester United. Drogba anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika kupata tuzo hiyo ambayo mwaka uliopita ilikuwa ikishikiliwa na mshambuliaji nyota wa klabu ya Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic.

No comments:

Post a Comment