Thursday, October 17, 2013

WAZIRI WA MICHEZO BRAZIL KUJIUZULU.

WAZIRI wa michezo wa Brazil, Aldo Rebelo anatarajiwa kujiuzulu Desemba mwaka huu ikiwa imebaki miezi sita kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia ambayo imeandaliwa na nchi hiyo. Rebelo amesema atajiuzulu nafasi hiyo ili aje mtu mpya baada ya kukabidhi viwanja 12 ambavyo vitatumika kwa ajili ya michuano hiyo, vinavyotarajiwa kukamilika Desemba. Mwaka uliopita Rebelo aliingia katika mzozo wa kidiplomasia na kugoma kuonana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Dunia-FIFA, Jerome Valcke baada ya katibu huyo kuponda maandalizi ya nchi hiyo na kudai kuwa wanahitaji msaada. Rebelo amesema sababu kubwa ya kujiuzulu ni kwa ajili ya kujiandaa ili aweze kuogombea kiti cha urais wa nchi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika Octoba mwakani.

No comments:

Post a Comment