Thursday, October 17, 2013

ABOUTRIKA KUTUNDIKA DARUGA.

MKONGWE Mohamed Aboutrika anayechezea klabu ya Al Ahly ya Misri anatarajia kutundika daruga mwaka huu. Kwa mujibu wa luninga ya Al-Ahly ,Aboutrika mwenye miaka 34 atastaafu baada ya Al Ahly kukamilisha kibarua chake kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika watakapochuana na Coton Sport ya Cameroon Jumapili ijayo katika mechi ya mkondo wa pili. Kama Al Ahly watafuzu watakutana na Esperance ya Tunisia au Orlando Pirates ya South Africa kwenye hatua ya fainali ya mikondo miwili itakayochezwa November mwaka huu. Mkongwe huyo ni mmoja wa wachezaji bora Africa ambaye hakuwahi kucheza Ulaya ambapo alikuwepo katika kikosa cha timu ya taifa ya Misri kilichogaragazwa na Ghana kwa mabao 6-1 katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kushiriki KOmbe la Dunia 2014.

No comments:

Post a Comment