Thursday, October 17, 2013

TANZANIA YAENDELEA KUSUASUA VIWANGO FIFA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora kwa mwezi huu huku Tanzania ikizidi kudidimia kwa kuporomoka kwa nafasi mbili. Katika orodha hizo Tanzania imeshuka mpaka katika nafasi ya 129 kutoka nafasi ya 127 waliyokuwepo mwezi uliopita. Kwa upande wa Afrika Ivory Coast wameendelea kuongoza kwa kushika nafasi ya 17 katika orodha hizo duniani wakifuatiwa na Ghana ambao wanashika nafasi ya 23 huku Algeria nao wakiwa katika nafasi ya 32. Mabingwa wa Afrika Nigeria wanashika nafasi ya nne kwa kushika nafasi ya 33 na tano bora kwa upande wa Afrika inafungwa na Mali walioko katika nafasi ya 41. Mabingwa wa dunia Hispania wameendelea kubaki katika nafasi ya kwanza kwenye orodha hizo wakifuatiwa na Ujerumani waliopanda mpaka nafasi ya pili na kuiondoa Argentina iliyopo katika nafasi ya tatu. Nafasi ya nne katika orodha hizo inashikiliwa na Colombia ambao wamepanda kwa nafasi moja kulinganisha na walipokuwa mwezi uliopita huku Ubelgiji wakifunga tano ya orodha hizo.

No comments:

Post a Comment