Wednesday, October 16, 2013

WORLD CUP 2014: UINGEREZA, MABINGWA WATETEZI HISPANIA WAJIHAKIKISHIA NAFASI YA BRAZIL MWAKANI.

WAKATI kampeni za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 zikikaribia tamati nchi saba zaidi jana zimejikatia tiketi ya moja kwa moja kwenda kushiriki michuano hiyo itakayofanyika nchini Brazil. Wenyeji Brazil tayari wameungana na japan, Australia, Iran na Korea Kusini kwa upande wa bara la Asia pamoja na Uholanzi, Italia, ujerumani, Ubelgiji na Switzerland kwa upande wa Ulaya, Argentina na Colombia kutoka Conmebol na Costa Rica na Marekani kutoka Concacaf. Nchi nyingine saba zilizoongezeka katika orodha hiyo baada ya mechi za jana usiku ni pamoja na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Hispania ambao walifanikiwa kushinda mechi yao dhidi ya Georgia kwa mabao 2-0, Uingereza na Urusi kwa upande wa Ulaya. Kwa upande wa Amerika Kusini Chile ilifanikiwa nayo ilifanikiwa kukata tiketi baada ya kuibugiza Ecuador kwa mabao 2-1, ingawa Ecuador nao walifuzu baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi hilo. Matokeo hayo ya jana yanapelekea nchi za Ureno, Ugiriki, Ukraine, Croatia, Romania, Sweden, Ufaransa na Iceland kucheza hatua ya mtoano ili kupata nafasi wakati Jordan watakwaana na Uruguay huku New Zealand wakicheza na Mexico katika hatua kama hiyo.

No comments:

Post a Comment