Tuesday, November 5, 2013

ALONSO KUSHIRIKI US GRAND PRIX PAMOJA NA KUWA MAJERUHI.

TIMU ya Ferrari imedai kuwa dereva wao nyota Fernando Alonso atakuwa fiti kwa ajili ya mashindano ya Grand Prix ya Marekani pamoja na kupata maumivu ya mgongo. Kulikuwa na wasiwasi kwamba Alonso mwenye umri wa miaka 32 asingeweza kushiriki mashindano hayo baada ya kupata ajali na kuumia mgongo katika mashindano ya Abu Dhabi Grand Prix. Alonso aliruhusiwa kutoka hospitali Jumapili lakini alifanyiwa uchunguzi zaidi Jumatatu baada ya tatizo la mgongo kujirudia. Msemaji wa Ferrari amesema Alonso amekuwa na maumivu madogo mdogo lakini yuko fiti na hana tatizo kubwa. Mashindano ya Grand Prix ya Marekani yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 17.

No comments:

Post a Comment