VIGOGO wa soka nchini Misri klabu ya Al Ahly wameshindwa kushawishi mamlaka ya kijeshi nchini humo ili kuhamisha mchezo wao katika Uwanja wenye uwezo wa kuingiza watu 70,000 ambao sasa watalazimika kucheza mechi yao ya mkondo wa ili ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Orando Pirates katika Uwanja wa Arab Contractors. Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 30,000 utapunguza madhara ya kuwa na mashabiki wengi watukutu wa Al Ahly lakini Pirates sasa itabidi wajipange vyema kutokana na nyasi za kuchezea kutokuwa vizuri. Wiki iliyopita Al Ahly walifanikiwa kuhamisha mechi hiyo jijini Cairo baada ya mabingwa hao mara saba wa michuano hiyo kuwa wakicheza mechi zao katika Uwanja wa El-Gouna uliopo nje ya mji wa Cairo kwa miezi kadhaa. Mamlaka ya kijeshi nchini Misri hawataki mechi yoyote kuchezwa katika mji mkuu wan chi hiyo toka rais Mohamed Mursi alipoondolewa madarakani JUlai mwaka huu kwa hofu ya kuogopa mkusanyiko mkubwa unaoweza kusababisha machafuko.
No comments:
Post a Comment