Tuesday, November 5, 2013

MOYES ATAKA JANUZAJ ALINDWE ZAIDI.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes anaamini kuwa nyota wake anayechipukia Adnan Januzaj anastahili kulindwa zaidi baada ya kukwatuliwa na beki wa Fulham Sascha Riether katika mchezo baina ya timu hizo mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa mara nyingine Januzaj alionyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo na kuisaidia United kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham. Riether ameshitakiwa kwa mchezo usio wa kiungwana na Chama cha Soka cha Uingereza-FA Jumatatu kwa kosa hilo na Moyes anataka hatua kali zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kumlinda kinda wake huyo. Moyes amesema Januzaj amekuwa akichezewa na mabeki hivyo kuhatarisha kipaji chake hivyo anadhani waamuzi wanapaswa kumchunga zaidi kinda huyo.

No comments:

Post a Comment