Tuesday, November 5, 2013

UINGEREZA HAIWEZI KUNYAKUWA KOMBE LA DUNIA NCHINI BRAZIL - ERIKSSON.

KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Sven-Goran Eriksson ameiondoa nchi hiyo katika nafasi ya kunyakuwa Kombe la Dunia litakalofanyika mwakani nchini Brazil. Eriksson mwenye umri wa miaka 65 ambaye sasa ni kocha wa timu ya Guangzhou R&F inayoshiriki Ligi Kuu nchini China, alioongoza Uingereza kufikia hatua ya robo fainali katika michuano ya Kombe la Dunia 2002 na 2006. Akihojiwa na BBC Eriksson amesema haamini kama Uingereza wanaweza kushinda michuano hiyo nchini Brazil labda Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Urusi mwaka 2018 kwasababu kuna wachezaji wengi vijana wanaochiukia hivi sasa. Uingereza ambayo inanolewa na Roy Hodgson hivi sasa tayari wameshafuzu kwenda nchini Brazil mwakani baada ya kuongoza kundi lao lakini katika ratiba ya michuano hiyo itakayopangwa Desemba mwaka huu Uingereza itakuwa katika timu za chaguo la pili.

No comments:

Post a Comment