Tuesday, November 5, 2013

UZOEFU NDIO UNAMUANGUSHA NEYMAR - PELE.

NGULI wa soka wa Brazil, Pele amesema mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona Neymar anakosa uzoefu ili kumlinganisha na Lionel Messi lakini amesisitiza tayari ni mchezaji aliyekamilika kwa kila kitu. Katika msimu wake wa kwanza akiwa Barcelona, Neymar mwenye umri wa miaka 21 amefunga mabao manne na kutoa pasi za mwisho nane katika mechi 15 alizocheza wakati Messi ameshafunga mabao 12 na kutoa pasi za mwisho nne katika mechi 14 alizocheza. Pele anaamini kuwa Neymar atakuja kuwa mmoja wa washambuliaji hatari zaidi duniani lakini anafikiri anahitaji muda zaidi ili kukuza kiwango chake barani Ulaya kabla ya kufikia huko. Pele aliendelea kudai kuwa kuna wachezaji wengi wazuri hivi sasa lakini katika chaguo la mchezaji bora wa dunia mpambano unakuwa kuwa kati ya Messi na Cristiano Ronaldo.

No comments:

Post a Comment