Saturday, November 16, 2013

BOATENG ATOA YA MOYONI KUHUSU BLACK STARS.

KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Ghana Kevin-Prince Boateng ameongea ya moyoni kufuatia mashabiki wa soka nchini humo kuona kama anaringa kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo. Nyota huyo anayecheza katika klabu ya Schalke ya Ujerumani alirejea tena kuitumikia timu yake ya taifa Agosti mwaka huu baada ya kustaafu kwa muda lakini bado hajacheza mechi yoyote ya kimataifa kutokana na majeruhi ambayo amekuwa akipata kipindi anachohitajika kuitumikia nchi hiyo. Boateng amesema sio kwamba huwa anaringa kuitumikia Black Stars lakini huwa anapata matatizo ya majeruhi kipindi ambacho ameitwa ndio maana ameshindwa kuwemo kwenye kikosi toka arejee Agosti. Boateng aliendelea kusema kuwa huwa anapenda kuwa fiti kwa asilimia 100 ili aweze kucheza kwa uwezo wake wote anapokuwa na Black Stars. Kwasasa Boateng yuko anafanya mazoezi na timu ya Ghana iliyopiga kambi nchini Uturuki ikijiwinda mechi yao ya marudiano dhidi ya Misri Jumanne. 


No comments:

Post a Comment