Saturday, November 16, 2013

RONALDO AISAIDIA URENO KUIFUNGA SWEDEN.

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo jana usiku aliisaidia timu yake ya Ureno kupiga hatua muhimu kuelekea kufuzu fainali za Kombe la Dunia Brazil baada ya kuifungia bao pekee katika mchezo wao dhidi ya Sweden. Kwa ushindi huo Ronaldo amembwaga mshambuliaji wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic anayeichezea PSG ya Ufaransa ambaye naye alikuwa anaoingoza timu yake katika mbio za kuelekea Brazil. Bao pekee la Ronaldo lilifungwa dakika ya 62 ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo huo na kuifanya Ureno kupata ushindi wa bao 1-0. Timu hizo zinatarajiwa kukutana tena katika mechi ya mkondo wa pili jijini Stockholm Jumanne ijayo ambayo ndio itakayoamua ni nani haswa atakaye kwenda nchini Brazil mwakani kwa ajili ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment