Saturday, November 16, 2013

YAYA TOURE, DROGBA WAONGOZA KATIKA ORODHA YA WACHEZAJI WALIOTEULIWA KUGOMBEA TUZO ZA CAF.


SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetoa orodha ya majina 25 ya wachezaji watakaogombe a tuzo ya mwanasoka bora mwaka 2013. Miongoni mwa majina hayo yupo Yaya Toure ambaye ni mshindi wa tuzo hizo kwa miaka miwli iliyopita pamoja na Didier Drogba wote wa Ivory Coast. Kama Toure anayekipiga katika klabu ya Manchester City akishinda tuzo hiyo mwaka huu atakuwa amefikia rekodi ya Samuel Eto’o wa Cameroon aliyeshinda tuzo hiyo kwa maika mitatu mfululizo yaani mwaka 2003, 2004 na 2005. Eto’o ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Chelsea ameshinda tuzo hizo mara nne lakini mwaka huu hakutajwa katika orodha hizo. Drogba mshindi wa tuzo hizo mara mbili ambaye sasa ancheza katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki na Gervinho anayecheza Roma ndio majina pekee ya wachezaji wa Ivory Coast huku Nigeria ikiingiza majina matano katika orodha hizo kutoka katika kikosi kilichonyakuwa Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu. Mshindi wa tuzo hizo atatangazwa katika hafla itakayofanyika jijini Lagos Nigeria Januari 9 mwakani. Orodha kamili ya wachezaji na nchi pamoja na timu wanazotoka ni Ahmed Musa (NGR/CSKA Moscow/RUS), Asamoah Gyan (GHA/Al Ain/UAE), Dame N'Doye (SEN/Lokomotiv Moscow/RUS), Didier Drogba (CIV/Galatasaray/TUR), Emmanuel Emenike (NGR/Fenerbahce/TUR), Islam Slimani (ALG/Sporting Lisbon/POR), John Obi Mikel (NGR/Chelsea/ENG), Jonathan Pitroipa (BUR/Rennes/FRA), Kevin Constant (GUI/AC Milan/ITA), Kwadwo Asamoah (GHA/Juventus/ITA), Luis Carlos Almada Soares 'Platini' (CPV/Omonia Nicosia/CYP), Mehdi Benatia (MAR/Roma/ITA), Mohamed Abou Trika (EGY/Al Ahly/EGY), Mohamed Salah (EGY/Basle/SUI), Nicolas Nkoulou (CAM/Marseille/FRA), Pierre-Emerick Aubameyang (GAB/Borussia Dortmund/GER), Ryan Mendes (CPV/Lille/FRA), Saladin Said (ETH/Wadi Degla/EGY), Seydou Keita (MAL/Dalian Aerbin/CHN), Sofiane Feghouli (ALG/Valencia/ESP), Sunday Mba (NGR/Warri Wolves/NGR), Victor Wanyama (KEN/Southampton/ENG), Vincent Enyeama (NGR/Lille/FRA), Gervinho (CIV/Roma/ITA), Yaya Toure (CIV/Manchester City/ENG)

No comments:

Post a Comment