Saturday, November 16, 2013

SAMATA ATAJWA TUZO ZA CAF.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samata ameendelea kung’ara zaidi katika anga za kimataifa baada ya kutajwa katika orodha ya wachezaji 21 watakaogombea tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara hili. Samata anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC amekuwa aking’ara na klabu hiyo kwa kufunga mabao katika mechi za ligi pamoja na michuano ya Kombe la Shirikisho. Mbali na Samata wachezaji wengine wanaocheza Mazembe waliotajwa katika orodha hizo ni pamoja na Reinford Kalaba kutoka Zambia na Tresor Mputu wa DRC. Wengine katika orodha hizo na nchi wanazotoka ni pamoja na Adane Girma (Ethiopia), Ahmed Fathi (Misri), Alex Kada (Cameroon), Ali Machani (Tunisia) Bapidi Fils Jean Jules (Cameroon), Daine Marcelle-Klate (Afrika Kusini), Ben Youssef (Tunisia), Getaneh Kebede (Ethiopia), Idrissa Kouyate (Ivory Coast) na Iheb Msakni (Tunisia). Wengine ni Luyanda Lennox Bacela (Afrika Kusini), Moez Ben Cherifia (Tunisia), Mohamed Abu Trika (Misri), Senzo Meyiwa (Afrika Kusini), Soumbeila Diakite (Mali), Sunday Mba (Nigeria), Waleed Soliman (Misri), na Yannick D’djeng (Cameroon).

No comments:

Post a Comment