Friday, November 15, 2013

MECHI TANO ZITAKAZOAMUA WAWAKILISHI WATANO WA BARA LA AFRIKA KATIKA KOMBE LA DUNIA 2014.

MACHO na masikio ya mashabiki wa soka barani Afrika yatakuwa yakitizama mechi tano muhimu zitakazochezwa Jumamosi, Jumapili na Jumanne ambazo ndio zitakazotoa wawakilishi watano watakaoliwakilisha bara hili katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Jumamosi tutashuhudia Ethiopia ikisafiri kuifuata Nigeria ili kujaribu kurekebisha makosa ya kufungwa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza wakati huko jijini Casablanca, Morocco, Senegal itaikaribisha Ivory Coast ambao walishinda mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Abidjan kwa mabao 3-1. Jumapili kutakuwa na mtanange mwingine wa kukata na shoka ambapo Tunisia wataifuata Cameroon jijini Younde baada ya kwenda sare ya bila ya kufungana katika mchezo wa kwanza uliofanyika Octoba. Ratiba hiyo itakamilika Jumanne ambapo Misri itakuwa na kibarua kigumu jijini Cairo cha kugeuza matokeo ya bao 6-1 walizochapwa na Ghana katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Kumasi wakati Burkina Faso nao wakijaribu bahati yao mbele ya Algeria baada ya kuwafunga mabao 3-2 katika mechi ya kwanza.

No comments:

Post a Comment