Friday, November 15, 2013

ETO'O ALALAMIKIA WACHEZAJI WENZAKE CAMEROON KUMBANIA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Chelsea, Samuel Eto’o anaamini kuwa baadhi ya wachezaji wenzake wa Cameroon wanajaribu kutomsaidia asishinde katika mechi yao ya mtoano ya Kombe la Dunia dhidi ya Tunisia. Kauli hiyo ya Eto,o imekuja wakati wakielekea katika mechi ya mkondo wa pili itakayofanyika jijini Younde baada ya ile ya kwanza iliyofanyika jijini Tunis Octoba timu hizo kwenda sare ya bila ya kufungana. Eto’o mwenye umri wa miaka 32 amedai kuwa wachezaji wenzake wamekuwa hawapeleki mipira ipasavyo anapokuwa mbele hivyo inampasa kurudi nyuma zaidi ili kwenda kutafuta mipira mwenyewe. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa soka ni mchezo wa ushirikiano na mchezaji ana jukumu la kutoa pasi hata kama unayempa mpira huo ni adui yako hususani unapokuwa katika nafasi nzuri. Hata hivyo, kocha wa Cameroon Volker Finke amepinga vikali madai hayo ya Eto’o na kusisitiza hakuona tatizo kama hilo wakati wa mchezo wao uliopita waliotoka sare.


No comments:

Post a Comment