Friday, November 15, 2013

KAKA YAKE MESSI AMNADI NDUGUYE, KUCHUKUA TUZO YA BALLON D'OR.

KAKA wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi ameingia katika kampeni ya kumnadi nduguye ili aweze kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or. Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya upigaji kwa ajili ya wanaogomea tuzo hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, nduguye nyota huyo aitwaye Matias Messi alituma picha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter ukiwa na picha ya Messi na Ronaldo pamoja na mataji waliyopata kuanzia mwaka 2009 mpaka 2013. 
Hata hivyo mshambuliaji wa Bayen Munich Franck Ribery anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo na kuwashinda Messi, Ronaldo pamoja na nyota wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic ambaye naye yuko katika kinyang’anyiro hicho. Kwasasa Messi amerejea nchini kwao Argentina kujiuguza baada ya kupata majeraha msuli ambayo yanaweza kumuweka nje kwa miezi zaidi ya miwili.

No comments:

Post a Comment