Friday, November 15, 2013

GHANA WAOMBA KUONGEZEWA ULINZI ZAIDI.

MAAFISA wa Shirikisho la Soka la Ghana-GFA limewaomba wenyeji wao Misri ulinzi zaidi kama tahadhari wakati timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Black Stars itakapowasili jijini Cairo wiki ijayo. Maofisa wanne kutoka GFA waliwasili jana Misri kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wan chi hiyo pamoja na kupata taarifa ya usalama pamoja na wawakilishi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Mjumbe wa bodi wa Shirikisho la Soka la Misri, Ehab Laheita ambaye alihudhuria mkutano huo amesema maofisa hao wa Ghana waliomba ulinzi zaidi wakati timu yao itakapowasili jijini Cairo na muwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani aliwahakikishia hilo. Laheita aliendelea kudai kuwa viongozi hao walikagua Uwanja wa Air Defense utakaotumika kwa ajili ya mchezo huo na kuridhishwa nao na kuomba nafasi zaidi kwa ajili ya mashabiki wao. Maofisa hao waliongozwa na rais wa GFA Kwesi Nyantakyi, Abeid Ayew Pele, Alhaji Saeed Lartey na Ibrahim Sannie.

No comments:

Post a Comment