Friday, November 15, 2013

WACHEZAJI CROATIA KUMWAGIWA FEDHA KAMA WAKIFUZU KOMBE LA DUNIA.

SHIRIKISHO la Soka nchini Croatia limetoa kitita cha euro 500,000 kama motisha kwa wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo kama wakifanikiwa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwakani nchini Brazil. Croatia inakabiliwa na mechi mbili za mtoano dhidi ya Iceland ili kukata tiketi kwa ajili ya michuano hiyo. Mechi ya mkondo wa kwanza kati ya timu hizo inatarajiwa kuchezwa jijini Reykjavik baadae leo huku mechi ya mkondo wa pili ikitarajiwa kuchezwa jijini Zagreb Jumanne ijayo. Croatia ilifanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1998 iliyofanyika nchini Ufaransa lakini walishindwa kufuzu michuano iliyopita ambayo ilifanyika nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment