Wednesday, November 6, 2013

DJOKOVIC AWEKA MATUMAINI HAI YA KUMALIZA NAMBA MOJA KWA KUMFUNGA FEDERER.

Nyota wa tenisi Novak Djokovic amefanikiwa kumfunga Roger Federer kwa mara ya pili ndani ya siku tatu na kumfanya kuanza vyema kutetea taji la michuano ya ATP World Tour. Djokovic raia wa Serbia Jumamosi iliyopita alimtandika Federer wa Switzerland katika nusu fainali ya michuano ya Paris Masters na kuweka matuamini yake hai ya kumaliza mwaka akiwa katika nafasi ya kwanza kwenye orodha za ubora duniani. Hata hivyo kama Rafael Nadal ambaye anakamata nafasi hiyo akimfunga Stanislas Wawrinka baadae leo atajihakikishia kumaliza mwaka katika nafasi hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Djokovic amesema umekuwa ni ushindi muhimu kwake haswa kutokana na kucheza mechi ngumu na muhimu ndani ya saa 48.

No comments:

Post a Comment