Wednesday, November 6, 2013

BAYERN, CITY ZAFUZU 16 BORA ULAYA.

MABINGWA watetezi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich na Manchester zimekuwa timu za kwanza kufuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo jana. Bayern walifanikiwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Viktoria Pilsen wakati mahasimu wao katika kundi hilo City wao walifuzu kwa mara ya kwanza hatua hiyo baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa misimu miwili iliyopita kwa kuitandika CSKA Moscow kwa mabao 5-2. Meneja wa Bayern, Pep Guardiola ambaye kikosi chake kimefikia rekodi iliyowekwa na Barcelona ya kushinda mechi tisa mfululizo katika michuano hiyo katika msimu wa 2002-2003,aliridhishwa na ushindi huo pamoja na timu hiyo kucheza katika kiwango cha chini. Guardiola amesema pamoja na kucheza chini ya kiwango lakini kitu cha msingi ni kuchukua alama zote muhimu katika mechi nne kitu ambacho kinaoenyesha jinsi gani walivyo hatari. Naye kocha wa City Manuel Pellegrini aliwaongeza wachezaji wake na kudai kuwa ulikuwa ni ushindi muhimu kwa timu ambayo haikuwahi kufuzu hatua hiyo huko nyuma.

No comments:

Post a Comment