Wednesday, November 6, 2013

BLATTER ATAKA KUONDOA HATUA YA MTOANO ILI KUFUZU KOMBE LA DUNIA.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter anataka kuondoa mechi za mtoano za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia huko mbele akidai kuwa ni hatua ngumu kupitia kwa timu kuikosa michuano hiyo. Mpaka sasa timu 20 pamoja na wenyeji Brazil ndio waliofuzu kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika mwakani kuitia hatua za makundi lakini nafasi 11 zilizobakia zitaamuliwa mwezi huu kwa mechi za mikondo miwili hatua ya mtoano. Mechi tano kati ya hizo zitachezwa barani Afrika wakati mechi zingine nne zitachezwa barani Ulaya huku zingine mbili zikipatikana katika mechi za mtoano za mabara. Blatter amesema atajaribu kutafuta utaratibu mwingine wa timu kufuzu lakini sio kufikia hatua ya mtoano kwasababu ni njia ngumu sana.

No comments:

Post a Comment