Wednesday, November 6, 2013

UNITED BADO INA NAFASI YA KUSONGA MBELE - GIGGS.

WINGA mkongwe wa klabu ya Manchester United, Ryan Giggs ana uhakika kikosi chake hicho kitasonga mbele katika hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kutoka sare ya bila ya kufungana na Real Sociedad. Nyota wa United Robin van Persie, Chicharito na Wayne Rooney wanapaswa kulaumiwa kwa matokeo hayoa baada ya kukosa nafasi kadhaa za wazi za kufunga kwenye mchezo huo ikiwemo penati iliyogonga mwamba ya Van Persie. Pamoja na sare hiyo United bado wanaongoza kundi A kwa alama moja zaidi baada ya Bayer Leverkusen na Shakhtar Donetski nao kutoka sare ya bila ya kufungana. Akihojiwa Giggs amesema anadhani walimiliki mchezo vyema dhidi ya Sociedad lakini amesikitishwa kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo huo. Lakini pamoja na hayo Giggs amesema hana shaka kwamba watasonga mbele kwasababu mechi yao inayofuata watacheza nyumbani.

No comments:

Post a Comment