Wednesday, November 6, 2013

GHANA WATAKA KUKUTANA NA BLATTER USO KWA USO.

VIONGOZI wa soka nchini Ghana wanapanga kukutana ana kwa ana na rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter ili kupata ufafanuzi wa usalama wa wachezaji, viongozi, mashabiki na waandishi wa habari watakaosafiri na timu ya taifa ya nchi hiyo kwenda Misri. Ghana inatarajiwa kucheza na Misri katika mechi ya mkondo wa pili ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 jijini Cairo, pamoja na Ghana kulalamikia hali ya usalama ya eneo hilo. Katika barua iliyosainiwa na Waziri wa Vijana na Michezo wan chi hiyo wamehoji maswali kwa shirikisho hilo kuomba ufafanuzi kuhusu usalama wao wakati wakisafiri kwenda huko na mpaka watakapocheza mechi yao. Waziri huyo amedai kuwa hawapingi maamuzi ya FIFA kuruhusu mechi hiyo ichezwe Cairo, lakini wanachosisitiza wao ni uhakika wa hatua gani zilizochukuliwa ili kudhibiti morari ya mashabiki wan chi hiyo baada ya matokeo yoyote ya mwisho wakati na baada ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment