Wednesday, November 6, 2013

AJUZA AFARIKI BAADA YA KUKIMBIA MARATHON YA KILOMETA 42 NA KUMALIZA.

BIBI kizee Joy Johnson wa Marekani ambaye alitengeneza vichwa vya habari Jumapili iliyoita kwa kuwa mwanamke mzee zaidi kukimbia katika mashindano ya Mrathon ya New York amefariki dunia Juzi. Bibi huyo mwenye umri wa miaka 86 mkazi wa eneo la San Jose jijini California ambaye alianza kupenda riadha katika umri mkubwa lakini akiwa ameshiriki mbio hizo za marathon kwa mara ya 25 mfululizo alianguka wakati akikaribia kumaliza mbio hizo. Pamoja na kupiga mweleka huo na kuumia kichwani bibi huyo aliendelea kukimbia na kumaliza mbio hizo za kilometa 42 akitumia masaa nane, na baadae kukataa kwenda hospitali kama alivyoshauriwa na watu wa huduma ya kwanza waliokuwepo. Jumatatu asubuhi Bibi huyo alionekana na dada yake Faith katika kipindi kimoja cha luninga na baada ya hapo wawili hao walirejea hotelini ambapo bibi Joy alijipumzisha na hakuamka tena mpaka lipotangazwa amekufa mchana wake.

No comments:

Post a Comment