Thursday, November 7, 2013

UEFA CHAMPINOS LEAGUE: HISPANIA YAINGIZA WATATU 16 BORA.

KLABU za Barcelona na Atletico Madrid zote za Hispania zimefanikiwa kutinga hatua ya timu 16 bora katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kushinda mechi zao jana usiku. Barcelona walisonga mbele baada ya kuwafunga mabingwa mara saba wa michuano hiyo AC Milan ya Italia kwa mabao 3-1 kwenye mchezo wa kundi H uliochezwa katika Uwanja wa Camp Nou. Atletico Madrid wao walisonga mbele baada ya kuibugiza Austria Vienna kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kundi G wakati Zenit Saint Petersburg ya Urusi ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuungana na Atletico walitoka sare ya bao 1-1 na Porto ya Ureno. Katika mechi nyingine iliyochezwa jana na kuvuta hisia za mashabiki wengi ilikuwa kati ya Borussia Dortmund ya Ujerumani waliokuwa wenyeji wa Arsenal ya Uingereza. Wenyeji Dortmund ambao walishinda katika mechi yao kwanza waliyokutana na Arsenal walishindwa kuendeleza ubabe kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 hivyo kufanya Arsenal kuongoza kundi F wakiwa na alama tisa sawa na Napoli ambao nao waliifunga Marseille kwa mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment