Thursday, November 7, 2013

BALOTELLI ANASTAHILI KUSUGUA BENCHI - ALLEGRI.

KOCHA wa timu ya AC Milan, Massimiliano Allegri amesisitiza kuwa Mario Balotelli alihitajika kuanzia katika benchi la wachezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Barcelona kwa manufaa ya timu na mshambuliaji huyo. Balotelli aliingizwa kama mchezaji wa akiba lakini alishindwa kubadili matokeo baada ya Milan kulala kwa mabao 3-1 yaliyofungwa na Lionel Messi na moja la Sergio Busquets. Allegri amesema Robinho alistahili kuanza katika mchezo huo badala ya Balotelli ambaye anaamini kuwa bado hajakuwa fiti kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimsumbua. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Balotelli aliumia akiwa katika majukumu ya kimataifa hivyo hakuona haja ya kumharakisha kumuingiza. Milan inashika nafasi ya pili katika kundi H lakini wamekuwa wakifanya vibaya katika Serie A na kujikuta wakiwa katika nafasi ya 11.

No comments:

Post a Comment